Mlipuko mkubwa ulitokea katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut ambao umeiharibu kabisa sehemu kubwa ya bandari na majengo katika maeneo mbalimbali ya mji huo.
Saa chache baadaye, magari ya kubebea wagonjwa yalikuwa yakiwabeba majeruhi huku helikopta za jeshi zikisaidia kuuzima moto mkubwa uliokuwa ukiendelea kuwaka katika bandari hiyo hapo jana jioni.
Waziri wa Afya wa Lebanon amesema vifo vilivyotokana na mlipuko huo vimefikia zaidi ya 70 huku majeruhi wakivuka 4000.
Vilevile waziri mkuu wa nchi hiyo amesema taarifa za awali zimeonyesha chanzo cha mlipuko huo ni kulipuka kwa Ammonium Nitrate Tani 2750 iliyohifadhiwa bandarini na inaaminika kemikali hiyo imelipuka kutokana na cheche za moto wakati wa kuchomelea mlango (welding).
Huku Rais wa Marekani Donald Trump akisema anaamini mlipuko uliotokea Beirut Lebanon ni shambulizi lililopangwa na kwamba bandari hiyo imelipuliwa kwa bomu au silaha nyingine nzito kwani ameongea na majenerali wa jeshi wa Marekani na mtazamo wao unaamini hilo ni shambulizi.