Kumekuwa na hali ya sintofahamu katika kijiji cha Kisungu ,Kaunti ya Kitui baada ya miili ya watu wawili kupatikana kichakani eneo hilo.Inaarifiwa kuwa wawili hao ambao ni mme na mke wake walipotea hapo jana walipokuwa wameenda kutafuta kuni eneo hilo.
Akidhibitisha tukio hilo chifu wa eneo hilo Patrick Katembu amewahimiza wakaazi kuwasaidia maafisa wa usalama na habari zitakazosaidia kubaini sababu kuu ya vifo vya wawili hao.
Miili ya wawili hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Kitui level 4 ikisubiri upasuaji