Polisi wamuua mshukiwa mmoja wa ujambazi kwa kumpiga risasi katika eneo la Mwiki, Kaunti ya Nairobi,nchini Kenya.Hii ni baada ya jaribio la wizi kutibuka.
Polisi wamesema kwamba mshukiwa alikuwa katika genge la washukiwa wengine wawili na walikuwa wanajaribu kuwaibia maafisa wa polisi waliyokuwa kwenye gari la kibinafsi na waliokuwa wamevalia nguo za raia.
Kulikuwa na makabiliano makali kati ya washukiwa wa ujambazi hao na polisi huku Polisi wakimpiga risasi mmoja wao na wengine wawili kutoroka kwa miguu.
Polisi walifanikiwa kupata bunduki moja ya kujitengenezea na risasi mbili kutoka kwa mshukiwa aliyeuawa.
Hali ya usalama imeimarishwa katika maeneo mengi huku shule zikifunguliwa nchini kote.