16.1 C
Nairobi
Sunday, September 26, 2021
Kenya
248,392
Total confirmed cases
Updated on September 26, 2021 8:39 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MSANII DIAMOND PLATNUMZ NA WCB WASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA KAMPUNI YA KIMATAIFA WARNER MUSIC

  Msanii maarufu na mfanyabiashara kutoka nchi ya Tanzania, Naseeb Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz ambaye pia ni mkurugenzi wa lebo ya WCB-Wasafi amesaini mkataba wa ushirikiano wa 360 wa kufanya kazi na Warner Music.

  Mkataba huo utaona yeye na wasanii wa WCB-Wasafi kwa jumla akijumuishwa katika Warner Music kwa lengo la kutangazwa zaidi ulimwenguni kupitia mtandao wao wa ulimwengu. Kwa maana hiyo,Diamond Platnumz,WCB-Wasafi na Warner Music watashirikiana kwenye matoleo mapya, katalogi, ushirikiano wa chapa, mikataba ya moja kwa moja na usawazishaji.

  “Kipaji cha muziki cha Diamond Platnumz hakiwezi kukanushwa na amekuwa mmoja wa wasanii waliofanikiwa zaidi barani Afrika……………………
  ….………………….Ushirikiano huo wa 360 unaanzisha njia mpya ya kushirikiana na wasanii barani Afrika na azma ya Warner Music kuleta talanta za Kiafrika kwa ulimwengu wote……..,’’ ilisema kampuni ya Warner Music.

  Warner Music group yenye makao makuu huko New York City, ni moja ya kampuni “kubwa tatu” za kurekodi na ya tatu kwa ukubwa katika tasnia ya muziki ulimwenguni, baada ya Universal Music Group na Sony Music Entertainment.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: