Mwanamziki wa nyimbo za injili amefunguka kuhusu muziki wake na malengo au vitu ambavyo anaazimia kuvifanikisha kupitia kwa muziki.
Akiongea na Mwandishi wetu Trizah B,Jane Alex amesema mojawapo ya vitu angetaka kufanikisha ni kumtumikia Muumba wake kupitia kwa muziki na pia kusambaza injili na jumbe za kuwatia moyo waliovunjika mioyo.
Vilevile Msanii huyo amesema ana azimio la kuwa msanii mkubwa wa nyimbo za injili huku akiwatia moyo watu duniani kote.
Pia ameweka wazi kuwa ameachia wimbo mpya kabisa unaoitwa NIBARIKI.
Ni wimbo ambao umetayarishwa kwenye studio za Champion Music iliyoko Nasra Estate jijini Nairobi na video kutayarishwa na Ray Mendosa Wa Claris Studio.
Msanii huyu ambaye ni mama na mke wa Alex Kironde,amewataja wasanii Size 8 na Mercy Masika kama watu anaowaangalia sana kwenye ulimwengu wa muziki yaani role models wake kuongeza kuwa mpaka sasa ameandika nyimbo zaidi ya 10 ambazo anatarajia kuachia moja baada ya nyingine.Hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kusubiri wimbo wa kuabudu ambao atauachia hivi karibuni lakini pia wasisahau kuingia YouTube watazame wimbo wake wa NIBARIKI.
Link ya kuutazama wimbo NIBARIKI hii hapa๐๐๐