Msanii wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto “Mjomba”, amepost picha kwenye mtandao wa kijamii ikimuonesha akiwa amevaa viatu huku akiuliza mashabiki zake kwamba aendelee kuvaa viatu au abaki kuwa peku.
Katika picha hiyo ambayo amepost kwenye ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa ameshaitwa mchawi, mshirikina kwa sababu ya imani yake ya kutembea peku au bila kuvaa viatu.
“Nimeitwa mchawi, mshirikina na masharti ya mganga kwa kutembea peku, hapo je? Nirudi peku au nibaki huku?” ameandika Mrisho Mpoto.
Ikumbukwe kwamba msanii huyo alijizolea umaarufu kutokana na style yake ya kutembea peku au bila kuvaa viatu popote pale iwe mtaani, studio, mikutano hata akiwa stejini kwenye matamasha na shughuli zingine za kimuziki.Hata hivyo Mrisho Mpoto kwa takriban miezi mitatu hivi amekuwa akijipost kwenye mtandao wake wa Instagram akiwa amevaa viatu ila hajawahi kuliongelea hilo mpaka hapo jana alivyo fanya hivyo.