14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 6:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MSANII WA NYIMBO ZA INJILI GUARDIAN ANGEL AKANA MADAI KUWA ANAMCHUMBIA MWANAMKE WA MIAKA 50

  Guardian Angel na Esther Musila wameongelewa sana kwa majuma mawili mitandaoni. Kumekuwa na fununu kuwa wawili hao wanachumbiana huku picha kadhaa zao wawili zikitapakaa mitandaoni wakiwa wamevalia nguo zinazofanana.Picha hizo zinaweza kufanya mtu yeyote kubashiri kuwa ni wapenzi wa dhati,madai ambayo Guardian amefutilia mbali.

  Mwanamuziki huyo wa nyimbo za injili Guardian Angel amefutilia mbali madai hayo kuwa anamchumbia mwanamke huyo wa umri wa miaka 50. Juma lililopita, wawili hao walizungumziwa sana mitandaoni ikisemekana Esther Musila ambaye ni mama wa watoto 3 wenye wako kati ya umri wa miaka 20 – 30 ni kipenzi cha msanii huyo.
  Akiwa kwenye mahojiano na Milele FM, Guardian amesema hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Esther hivyo ni rafiki wa karibu na pia shabiki wake sugu.

  “Esther ni shabiki wangu, mimi huwapenda mashabiki wangu wote, yeye pia ni rafiki wa karibu na mara nyingi sisi hushinda Pamoja,…… wajua mimi ni mhubiri,……… Mimi huwa sifanyi biashara ya siri, nikiwa na mchumba nitamtambulisha kwa wakati wake’’ Alisema Guardian.

  Hata hivyo Mwandishi wetu wa www.vuvu.co.ke amekuwa akifuatilia matukio yao kwenye mitandao yao ya kijamii.Kutokana na posts za wawili hao,kuna uwezekano ni kiki ya kuachia wimbo wao unaotarajiwa kuachiwa wakati wowote kutoka sasa kwani Siku 6 zilizopita Guardian amepost picha kwenye mtandao wake wa Instagram na kuandika, ‘’Another from @ngenyi .. and I.. #HARUSI coming soon hii nayo watu watakatika kweli kweli…
  #coming soon .. MUSIC DOCTOR .ft . ESTHER.’’ Huku akiambatanisha na poster ya wimbo uitwao HARUSI.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: