Maafisa wa idara ya upelelezi jijini Nairobi nchini Kenya wamemkamata mshukiwa mmoja wa mauaji.
Leonard Kamanga Kamau anasemekana kumuua kinyama mfanyakazi wa nyumbani jijini Nairobi katika mtaa wa Umoja mnamo tarehe 19/3 mwaka huu.
Mwili wa Tabitha wanjiku mwenye umri wa miaka 25 ulipatikana na wapangaji wengine wa nyumba huku ukiwa umekatakatwa kooni kwa kisu.
Aidha Kamau kwa sasa ameshikiliwa na polisi akisubiri kufikishwa mahakamani mnamo jumatatu ijayo.