‘’Huenda wanafunzi wakaendelea kusalia nyumbani mwaka huu wote nchini Kenya na isijulikane siku maalum ya kuzifungua shule,’’ hii ni kauli ya Waziri wa Elimu,Profesa George Magoha akiongea mbele ya kamati ya Bunge la Kitaifa mwezi mei 2020.Huku Tanzania hivi sasa ikiwa imefungua shule zote na masomo yanaendelea kama kawaida.
Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt Charles Msonde, mitihani ya kidato cha sita itaanza leo Jumatatu 29,2020.Huku jumla ya watahiniwa 85,546 ndiyo waliosajiliwa kufanya mitihani hiyo ya kidato cha sita na ualimu inayotarajiwa kuanza nchi nzima leo Jumatatu .
Msonde amesema maandalizi yote yameshakamilika.
Aidha baraza pia limezitaka kamati za mikoa za kusimamia mitihani kuhakikisha wanasimamia mitihani hiyo na kusitokee udanganyifu wowote kwa watahiniwa.