22 C
Nairobi
Monday, April 19, 2021
Kenya
151,653
Total confirmed cases
Updated on April 19, 2021 12:09 pm

MBUNGE WA JUJA FRANCIS WANYUA WAITITU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MREFU

Mbunge wa Juja nchini Kenya, Francis Munyua Waititu amefariki dunia. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia yake ambayo ilithibitisha kifo chake, Waititu maarufu...
More

  Latest Posts

  MWALIMU ALIYEMKATA PANGA MWALIMU MWENZAKE MZOZO WA PENZI LA MWALIMU MWANAFUNZI WA FIELD AFIKISHWA MAHAKAMANI

  Mwalimu wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Karoti katika Kaunti ya Mwea Mashariki nchini Kenya, Timothy Musembi (34) ambaye alimshambulia na kumjeruhi mwenzake aitwaye Alphonce Orina (26) wakizozania penzi ameshtakiwa kwa jaribio la mauaji.

  Inasemekana mnamo Machi 2,2021 , Orina alikuwa ofisini wakati mwenzake aliingia akiwa amejihami kwa panga na kuanza kumshambulia akimzomea kwa kumnyemelea mwalimu wa kike ambaye yuko kwenye mazoezi ya kufundisha shuleni hapo.

  Alimkata mara mbili kichwani na kumlaazimu Orina kujitetea kwa vita naye.Katika hali hiyo ,Orina alijeruhiwa vibaya mikononi wakati alipokuwa akijaribu kujizuia dhidi ya makali ya panga ya mwenzake.Mwathiriwa alizidiwa na kuanguka chini ambapo walimu wengine walilazimika kuingilia kati na kumkimbiza hospititalini.

  Picha ya Mwalimu aliyekatwa panga na mwalimu mwenzake

  Baadaye mshukiwa alijisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Wang’uru ambapo alizuiliwa kabla ya kufikishwa mahakamani Alhamisi Machi 4, 2021 akiwa chini ya ulinzi mkali ambapo alitakiwa kujibu kosa la jinai.

  Mahakama iliarifiwa kuwa shambulio hilo lililotokea afisini, mwathirwa alipata majeraha mabaya na ilibidi alazwe hospitalini kwa matibabu maalum.

  Mshukiwa alipofika mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Monica Kivuti, alikanusha shtaka hilo na kuomba aachiliwe kwa dhamana.

  Ambapo Hakimu Mkazi Mwandamizi Monica Kivuti, aliamuru aachiliwe kwa dhamana ya KSh100,000 hadi Machi 17 kesi hiyo itakapotajwa.

  Hata hivyo, mshtakiwa alitupwa kizuizini kwani alishindwa kulipa hela hizo.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: