22 C
Nairobi
Monday, April 19, 2021
Kenya
151,653
Total confirmed cases
Updated on April 19, 2021 12:09 pm

MBUNGE WA JUJA FRANCIS WANYUA WAITITU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MREFU

Mbunge wa Juja nchini Kenya, Francis Munyua Waititu amefariki dunia. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia yake ambayo ilithibitisha kifo chake, Waititu maarufu...
More

  Latest Posts

  MWANAFUNZI WA MIAKA 14 AUAWA NA MWILI WAKE KUTUPWA KICHAKANI

  Mwanafunzi wa darasa la nne aliyejulikana kwa jina Bhoke Keroche aliyekuwa anasoma katika shule ya msingi Kemarambo wilayani Serengeti  mkazi wa kijiji cha Ring’wani amefariki katika mazingira ya kutatanisha.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Ring’wani,Julius Kibure ni kwamba mwili wa mwanafunzi huyo mwenye umri wa 14, anayeaminika kuuawa Februari 28, 2021,ulikutwa kwenye kichaka Machi Mosi, 2021  baada ya msako mkali.

  Bhoke anadaiwa   kuuawa na mtu aliyeajiriwa kwa ajili ya kuchunga mifugo ya familia yake takribani mwezi mmoja uliopita.

  Mkuu wa Wilaya ya Serengeti,  Nurdin Babu amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama wanaendelea kumsaka mtuhumiwa aliyemtaja kwa jina la Issa Msukuma.

  Daktari mkuu wa hospitali teule ya Nyerere, Tanu Warioba amesema mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika hospitali hiyo.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: