22.8 C
Nairobi
Friday, October 15, 2021
Kenya
251,669
Total confirmed cases
Updated on October 14, 2021 9:34 pm

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MWANAFUNZI WA MIAKA 17 AJIFUNGUA NA KUMUUZA MWANAWE KWA SH 3000

  Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha 2 amewashangaza wengi alipojifungua na kumuuza mwanawe kwa ksh 3000 akishirikiana na mamake mzazi.baada ya babake kumfukuza nyumbani kwao Butere katika kaunti ya kakamega nchini Kenya.
  Kwa mujibu wa msichana huyo alipachikwa mimba na jamaa wa ukoo wake hali iliyopelekea babake kumfukuza kutoka nyumbani na kuenda kuishi na mamake ambaye anaishi katika nyumba ya kukodi mjini Butere.
  Mamake mwanzo alikuwa amemshauri amnyonge mtoto pindi atakapozaliwa ila baadaye akabadili nia hiyo.Mtoto alipozaliwa Ijumaa iliyopita mamake akatafuta na kumpata mnunuzi wa mtoto huyo na kumuuza kwa shilingi 3000.
  Mamake mtoto huyo anasema kwamba kando na mila za kwao ambapo mtoto huyo anafaa kuuawa lakini kutokana na hali yake ngumu ya maisha ilimfanya kumuuza mjukuu wake.
  Naibu chifu wa eneo hilo Hesbon Ndunde amesema wanaendelea kumsaka mama aliyemnunua mtoto huyo.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: