19.4 C
Nairobi
Saturday, October 16, 2021
Kenya
251,669
Total confirmed cases
Updated on October 14, 2021 9:34 pm

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MWANAMFALME PHILIP, MUME WA MALKIA WA UINGEREZA AMEFARIKI DUNIA

  Mwanamfalme Philip, mume wa Malkia Elizabeth II, amefariki dunia Ijumaa asubuhi April 9, 2021.
  Kwa mujibu wa ujumbe kutoka kwa familia ulioandikwa kwenye mtandao wa Twitter Ijumaa, Aprili 9, marehemu, mwenye umri wa miaka 99 akiwa amebakisha miezi miwili afikishe miaka 100, aliaga dunia kwa amani asubuhi katika Jumba la Windsor.

  “Ni kwa huzuni kubwa kwamba Malkia ametangaza kifo cha mumewe mpendwa, Mwanamfalme Philip, Duke wa Edinburgh,” sehemu ya ujumbe huo ilisema.

  Mwanamfalme Philip alimuoa Elizabeth mwaka 1947, miaka mitano kabla ya kuwa Malkia.

  Picha ya Harusi ya Elizabeth na Philip kabla ya Elizabeth kuwa Malkia

  Mwanamfalme Philip na Malkia Elizabeth wa uingereza Walikuwa na watoto wanne ,wajukuu wanane na vitukuu 10.

  Kifo chake Mwanamfalme huyo kimetokea mwezi mmoja baada ya kutolewa katika hospitali binafsi aliyokuwa amelazwa kwa wiki mbili na kuhamishiwa katika hositali nyingine mjini London ili kufanyiwa vipimo vya moyo na matibabu zaidi.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: