Polisi jijini Nairobi wanafanya uchunguzi ambapo mwanamke wa miaka 42 alifariki dunia baada ya kulala na ndugu wa kiume wa mume wake gesti usiku kucha.
Kulingana na ripoti ya polisi, John Kisongona Mareko aliwasili jijini Nairobi Jumatano, Septemba 23,2020 saa moja ya jioni kutoka Malindi na kumualika mke wa nduguye Jesca Sibwe aliyekuwa anaishi eneo la Kasarani ambapo wawili hao walilala gesti katika hoteli ya Graceland iliyoko Dubois jijini Nairobi
Inasemekana mwanamke huyo (Jesca Sibwe) alianza kukohoa na ndiposa wakaitisha teski ya kumkimbiza katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta ambapo madaktari walithibistisha tayari alikuwa amekata roho.
Mwili wake ulipelekwa katika makafani ya hospitali hiyo kusubiri upasuaji huku maafisa kutoka Idara ya Upelelezi wakianzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.