18.4 C
Nairobi
Saturday, May 8, 2021
Kenya
162,666
Total confirmed cases
Updated on May 8, 2021 11:18 am

GAVANA WA ZAMANI WA NAIROBI MIKE SONKO AACHILIWA KWA DHAMANA

Hatimaye aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ameachiliwa kwa dhamana baada ya kuzuiliwa rumande kwa muda wa takribani mwezi mmoja. Kwa mujibu wa TUKONEWS, Sonko...
More

  Latest Posts

  MWANAMKE ATEKETEZA MAKAAZI YAO AKIMLAUMU MUMEWE,BUNGOMA

  Mwanamke mmoja ameteketeza nyumba yao na kila kitu ndani ya nyumba hiyo kuchomeka katika soko la Misihu katika Kaunti ya Bungoma nchini Kenya .Inaarifiwa kuwa mzozo wa nyumbani umesababisha mwanamke huyo kwa jina Alice Masinde kuteketeza makaazi yao.
  Kwa mujibu wa Elijah Monjeru ambaye ni mume wa Alice Masinde ni kwamba mkewe amekuwa na hulka ya kulewa kupindukia bila kujali familia yake.Alice amekuwa akichukua vyombo vya nyumbani na kuuza kwa ajili ya kununua pombe na kuharibu vingine.
  Hata hivyo Elijah ameongeza kwamba mkewe amekuwa akiwaacha watoto bila chakula na kuenda kulewa.
  Mwanamke huyo amekiri kuteketeza nyumba yao japo amemtuhumu mumewe kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine.
  Mmoja wa wakkazi katika soko la Misuhu amemlaumu mwanamke huyo akisema kwamba amekuwa akiwahangaisha wakaazi katika soko hilo kwa kujifanya kama wazimu na si wazimu na kuiomba serikali kuingilia kati na kumsaidia mwanamke huyo ili kumuokoa kutoka kwa uraibu wa ulevi.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: