Nyota wa muziki Suzanna Owiyo kutoka Kenya alitangaza habari hizo za kuvunja moyo kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram alimtaja marehemu kuwa mshauri wake mkuu kando na kuwa babake.
Ujumbe huo aliyo uandika Kwa lugha ya Kingereza ulisoma kwa tafsiri, ” Ni vigumu sana kukuaga kwa heri ila najua upo mahali pema kwa sasa na uko na amani , nitakukosa sana na utazidi kuwa moyoni mwangu, asante kwa kuwa baba mzuri na mshauri mkubwa kwa wengi, lala salama Dad.”
Mashabiki na marafiki walimuombeleza na wengi wameahidi kuiweka familia kwa maombi wakati huu wa huzuni na majonzi.
Hata hivyo, chanzo cha kifo cha babake Owiyo bado hakijabainika na hata mipango ya mazishi haijatangazwa.Nyota huyo wa Benga ambaye amevuma kwa vibao kadhaa ikiwemo ya ‘Kisumu 100’, ni mzaliwa wa kijiji cha Kasayo kule Nyakach