14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 7:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MWANAUME AFIA GESTI KWA KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME AKIFANYA MAPENZI NA MREMBO

  Mwanaume mmoja mwenye miaka 42, kutoka mjini Kakamega nchini Kenya ameaga dunia asubuhi ya Jumatano, Juni 24, 2020 baada ya kudaiwa kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume ‘Viagra’ kupita kiasi.

  OCPD wa Kakamega ya kati, David Kabena, amesema mwathiriwa aliyetambuliwa kama Munala, alikodisha chumba cha gesti mjini humo pamoja na mwanamke mmoja mwenye miaka 31, aliyetambuliwa kwa jina Anyango, kutoka Kaunti ya Siaya Jumanne, Juni 23,2020 mchana.

  Wawili hao waliagiza chakula cha jioni kabla ya kuelekea chumbani katika hoteli ya Amazon huku jamaa huyo akikosa kula chochote.Mapema Jumatano asubuhi, Anyango alitoka chumbani humo na kumuambia meneja wa hoteli hiyo kuwa mpenzi wake aliaga dunia baada ya kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume(viagra) kupita kiasi.

  Mkuu wa hoteli hiyo aliwaita maafisa wa polisi, ambao waliwasili na kuupeleka mwili wa mwanaume huyo katika makafani ya Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kaunti ya Kakamega ambapo ulifanyiwa upasuaji Jumatano mchana.
  Matokeo ya upasuaji yalionyesha kuwa marehemu aliaga dunia kutokana na mshtuko wa moyo ambao inaaminika kusababishwa na dawa hizo.

  Mwendazake alikuwa ameoa na kujaliwa mtoto wa kiume mwenye miaka 8, pamoja na mke wake ambaye wameishi pamoja kwa miaka kumi.Mjane wa jamaa huyo alisema hajafanya mapenzi na mume wake kwa mwaka mmoja sasa. OCPD alisema bado uchunguzi zaidi unaendelea kuhusu kifo cha mwanaume huyo.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: