16.1 C
Nairobi
Sunday, September 26, 2021
Kenya
248,392
Total confirmed cases
Updated on September 26, 2021 9:40 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MWANAUME AKATWA SHINGO NA MPENZI WA MKEWE

  Maafisa wa Polisi wamemkamata mvulana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na minane katika kaunti ya Nakuru kwa madai ya kumuua mwanaume wa miaka thelathini na miwili.

  Inadaiwa mshukiwa alimuua Denis Kioko kwa kumkata shingo katika mtaa wa Moi  South Lake baada ya kutofautiana kuhusu mwanamke.

  Kulingana na majirani Marehemu Kioko alifika nyumbani kwa mshukiwa na kumkaripia kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe mwenye umri wa miaka thelathini na mitano.

  Mkuu wa Polisi katika eneo hilo Samuel Waweru amesema wakati wa makabiliano hayo mshukiwa alijeruhiwa na marehemu na anatibiwa katika hospitali ya Rufaa ya Naivasha na atakamatwa atakaporuhusiwa kuondoka hospitali.

  Hata hivyo,mwili wa Kioko umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hosptali hiyo hiyo.

  Wakati huo huo ,baba amuua mwanawe kwa madai ya kujoa kitandani katika eneo la Bondo katika kaunti ya Siaya, nchini Kenya.

  Maafisa wa polisi wanachunguza kisa hicho mwanamme huyo amemuua mwanawe wa kambo mwenye umri wa miezi kumi na kuutupa mwili wake chini ya kitanda.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: