14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 5:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MWANAUME AMKANA “AMRUKA” MKE WAKE PEUPE ASIMUUDHI MCHEPUKO

  Mwanaume mmoja awashangaza watu alipomkana mkewe hadharani ili asimkasirishe mpango wa kando au mchepuko. Inasemekana mwanaume huyo alikuwa akila raha na msichana ‘mchepuko’ huyo kabla ya mkewe kufika na kuwafumania alipopashwa habari mtaani.

  Inasemekana, mwanaume huyo alikuwa amepokea bonasi ya kahawa siku chache kabla ya kisanga hicho kutokea. Mkewe alipofahamishwa mmewe alipokuwa akijivinjari na mpango wa kando, alielekea huko na kuwapata peupe wakibugia vileo na kupapasana.

  Taarifa zinasema kwamba mama huyo alianza kupiga nduru akilia na kumlaumu mumewe kwa kumwachia familia changa na kutorokea mjini kuponda raha na michepuko.

  Ili kuepuka kumkera mrembo huyo mwanaume alisimama na kumkemea mkewe akimtaka aondoke akidai hamjui. Waliokuwa eneo hilo la burudani walitazama jinsi jamaa alivyomkana mkewe hadharani ili kufurahisha mpango wa kando.

  Inaarifiwa kwamba waliomjua jamaa walimkemea vikali kwa kumkana mkewe hadharani.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: