Mwanaume wa makamu na mpenzi wake mwanamke mwenye umri wa miaka 23 wanazuiliwa kwenye Kituo cha Polisi cha Bomet mjini kutokana na madai kwamba mwanaume huyo amemnajisi na kisha kumuua mtoto wa mpenziwe huyo.
Mtoto aliyenajisiwa ana miaka mitatu na kisa hicho kimeripotiwa kutokea kwenye kijiji cha Kabisoge viungani mwa mji wa Bomet .Na kulingana na mkuu wa polisi eneo la Bomet ya kati/central Musa Imamai ,Mwanaume huyo ambaye ni mshukiwa,kwa jina Nathan Cheriyot inadaiwa alijifungia ndani ya nyumba na mtoto huyo kumnajisi kisha kumuua wakati mamake alikuwa amekwenda dukani.
Kwa mujibu wa majirani,wanaamini kwamba mwanamme huyo ambaye si baba mzazi wa mtoto mwahasiriwa pengine alikuwa na nia ya kumuua huyo mtoto ili amuoe mama bila mtoto.
Kulingana na polisi mshukiwa atafanyiwa uchunguzi wa akili kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.