Polisi katika eneo la Kitengela kwenye County ya Kajiado nchini Kenya wameanza msako dhidi ya mwanaume mmoja anayedaiwa kumuua mpenzi wake.Inadaiwa kwanza mshukiwa alimuua mpenziwe kwa kumnyonga jana usiku .Na kumuagiza mhudumu wa bodaboda kuupeleka mwili hadi katika msikiti wa chang’ombe japo alihadaiwa kwamba vilikuwa bidhaa za matumizi nyumbani ambazo muda wake wa matumizi ulikuwa umekamilika.
Mshukiwa aliufunga mwili huo kwenye malazi na kuuingiza kwenye mfuko wa plastiki.hata hivyo walitofautiana na mhudumu wa bodaboda ambae alishuku kuhusu kilichopo ndani ya mfuko.Hali hiyo ilimfanya mshukiwa kutoweka.
Polisi walijulishwa kuhusu kilichotokea na kubainika kuwa msichana aliyeuliwa ni mwenye miaka 20 hivi ambaye alikuwa akiishi na mpenzi wake huyo katika nyumba moja mtaani Kitengela kwa kipindi cha wiki mbili sasa.
Hata hivyo hakuna kilichopatikana kwenye nyumba ya mshukiwa.Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi eneo hilo.Mwili wa msichana huyo umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha City na kufikia sasa chanzo cha mauaji hayo hakijabainika.