16.1 C
Nairobi
Sunday, September 26, 2021
Kenya
248,392
Total confirmed cases
Updated on September 26, 2021 7:39 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MWANAUME AMUUA MWANAUWE MWINGINE BAADA YA KUMPATA LODGING NA MKE WAKE NA KUMSHAMBULIA MKEWE KWA KISU


  Polisi katika kaunti ya Bomet wanachunguza kisa ambapo mwanaume wa makamo ameuawa kwa kudungwa kisu na mshukiwa anayedaiwa kuwa mme wa mwanamke ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi.
  Inaarifiwa mhasiriwa ameshambuliwa kwa kisu akiwa ndani ya chumba cha wageni ‘ lodging’ katika kituo cha biashara cha Kapkwen katika viunga vya mji wa Bomet mvutano ukiwa juu ya mapenzi kwani madai yameibuka kuwa mhasiriwa alikuwa na uhusiano wa mapenzi na mke wa mshukiwa.
  Kamishna wa kaunti ya Bomet ,Naomi Ichami amesema mwanamke mhusika amelazwa katika hospitali ya Longisa akiwa na majeraha ya kisu mgongoni baada ya kuponea kifo kwani alishambuliwa pia walipopatikana wawili ndani ya lodging.
  Mshukiwa baada ya kuwashambulia wawili hao alijisalimisha kwenye kituo cha polisi cha Bomet mjini ambapo anasubiri kufikishwa mahakamani.
  Mwili wa mwanaume aliyeuawa umehifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Longisa.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: