Polisi katika eneo la Athi River jimbo la Machakos nchini Kenya,wanachunguza kisa ambacho mwanaume aitwaye Ernest Kamanda mwenye umri wa miaka 52 alizimia na kuaga dunia Jumatano, Februari 3,2021 usiku nyumbani kwa mwanamke.
Inasemekana Ernest Kamanda alianza kukumbwa na matatizo ya kiafya majira ya saa 11:30 jioni Jumatano wakiwa nyumbani kwa mwanamke aitwaye Catherine Kinyanjui mwenye umri wa miaka 47, ambapo alikimbizwa hospitali ya Shalom Community na majirani ambapo alisemekana tayari alikuwa amefariki dunia.
Kulingana na ripoti ya polisi,maafisa wa polisi waliwasili eneo la tukio kutathimni kilichotokea huku mwili wake ukihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo kusubiri upasuaji.