Kitengo cha dharura cha shirika la huduma za Ferry kimefanikiwa kumuokoa mwanaume aliyejirusha baharini katika kivuko cha Likoni jijini Mombasa nchini Kenya leo asubuhi .Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 54,alijirusha mapema leo asubuhi alipokuwa ameabiri Ferry ya MV Kwale.
Hata hivyo sababu za mwanaume huyo kuchukua hatua hiyo bado haijabainika.Tayari mwanaume huyo amekabidhiwa maafisa wa kituo cha Polisi cha Ferry ambapo atahojiwa.