14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 7:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MZEE MGONJWA WA MIAKA 68 AFUNGIWA NDANI YA NYUMBA NA MWANAE NA NDUGU YAKE KWA MIAKA MINNE KISA URITHI WA MALI ZAKE

  Mzee mmoja wa miaka 68, ameokolewa na maafisa wa polisi nchini Kenya.Mzee huyo,Emmanuel Ole Turere amekuwa akifungiwa ndani ya nyumba katika kijiji cha Ololoito eneo la Narok Kaskazini kuanzia mwaka wa 2014 hadi sasa ili asipate matibabu baada ya yeye kupata ajali na kupoteza uwezo wa kutembea.

  Kwa mjibu wa afisa mkuu wa polisi wa eneo hilo la Narok Kaskazini,Fredrick Shiundu amesema kuwa mbali na kumuokoa mzee huyo Emmanuel Ole Turere ambaye aligongwa na gari,wameweza pia kumkamata nduguye mzee huyo na kijana wake ambao ndio wamekuwa wakihusika katika kumfungia asipate matibabu kwa lengo la wao kurithi mali zake.

  Pia inasemekana kuwa wawili hao wamekuwa wakimzuia binti wa mzee huyo fursa ya kumuona na vilevile kumshughulikia kupata matibabu baada ya mamake mzazi kuaga dunia.

  Hivyo wawili hao watashtakiwa kwa makosa yao na mzee huyo Emmanuel kwa sasa yuko hospitalini akipokea matibabu.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: