Mwili wa mzee mmoja wa umri wa miaka 57 ambaye anakisiwa kujiua kwa kunywa sumu umepatikana ndani ya miti karibu na nyumbani kwake katika kijiji cha Nyambogo ,kata ya North Kitutu kule Manga kaunti ya Nyamira nchini Kenya.
Akithibitisha kisa hicho chifu katika eneo hilo Duke Mogaka,amesema kuwa marehemu Meshack Orina alitoweka kutoka nyumbani kwake jana jioni ambapo jamaa zake walimtafuta bila mafanikio hadi leo asubuhi walipopata mwili wake ndani ya miti hiyo kandokando na chupa ya dawa ya ng’ombe.