Wazee wa jamii ya Bukusu katika kijiji cha Wabuhonyi eneo bunge la Kimilili nchini Kenya,wanapania kufanya tambiko la kumtakasa mzee mmoja anayedaiwa kupatikana akila uroda na mkaza mwana.(Mke wa mwanae).
William Mahanu mwenye umri miaka (84) alipatikana na mkaza mwana wake chumbani mwake usiku wa kuamukia jumatatu hii.Akithibitisha kisa hicho mwanawe William,Wanjala anasikitika na tukio hilo na kudai kuwa huenda wakamfurusha baba yao kutoka kijiji hicho.
Inasemekana kuwa walimrai mzee huyo atoke nje ili wampe adabu ya viboko ishirini lakini akakataa kutoka nje kabla ya maafisa wa polisi kuwasili na kumuokoa.Kulingana na Gerald Baraza mzee wa jamii ya wabukusu itawabidi kuandaa tambiko la kuwatakasa mzee huyo Pamoja na mkaza mwana wake huyo ili kuepuka laana katika familia yake
Kwa sasa mzee huyo William ameshikiliwa katika kituo cha polisi cha Kamukuywa huku uchunguzi zaidi ukiendelea.