Wafanyakazi wa afya nchini Lesotho,wamekutana na kisa chao cha kwanza cha covid 19.Wizara ya afya ya nchi hiyo ilidhibitisha kisa hicho cha kwanza Jumatano hii na kuifanya nchi hiyo kuwa ya mwisho katika nchi 54 kwenye bara la Afrika kuripoti ugonjwa huo.
Mamlaka nchini humo ilisema mgonjwa huyo ambaye kwa sasa ametengwa alipimwa na kukutwa na ugonjwa huo baada ya kuingia nchini Lesotho siku sita zilizopita lakini hakuonyesha dalili zozote. Mgonjwa huyo alikuwa mmoja tu kati ya wengi waliosafiri kutoka Saudi Arabia na Afrika Kusini kukutwa na ugonjwa huo.