14.8 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 8:34 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  OMBI LA KUFUTA KESI YA JARIBIO LA MAUAJI DHIDI YA BABU OWINO LIMEKATALIWA NA MAHAKAMA

  Mahakama mjini Nairobi Machi 15,2021, ilitupilia mbali ombi la kutupilia mbali kesi ya jaribio la mauaji dhidi ya Mbunge wa Embakasi Mashariki nchini Kenya ,Babu Owino.

  Felix Orinda maarufu DJ Evolve ambaye ndiye alipigwa risasi na mbunge huyo, aliiomba mahakama kutupilia mbali kesi dhidi ya mbunge Babu Owino kwa madai kwamba amemsamehe na anataka kuangazia uponaji wake.

  Picha ya DJ evolve akiwa Kitandani

  Hakimu Mkuu Bernard Ochoi amesema kuwa kujiondoa tu mwenyewe sio jambo stahiki katika kesi ambayo mbunge huyo anashitakiwa kwa makosa ya kumpiga risasi Felix Orinda maarufu kama DJ Evolve.Na hivyo ombi hilo halikufikia mahitajika yanayotakikana ili kesi hiyo iweze kutupiliwa mbali kwa sasa.

  Hakimu Ochoi amesema ingawa bado fursa ya majadiliano zaidi iko wazi ila hawezi kutupilia mbali kesi hiyo kwa sasa kwa sababu hajui Babu Owino amempa nini DJ Evolve.

  “Kujiondoa tu mwenyewe sio sahihi katika hali kama ya kesi hii; wahusika wote wanastahili kujitokeza wazi kuambia mahakama kile ambacho Babu ametoa kwa ajili ya familia,” Ochoi amesema.
  Mwaka jana mbunge huyo alishtakiwa kwa makosa ya jaribio la kuua kwa kukusudia dhidi ya DJ Evolve katika klabu maarufu B ambapo baadae aliachiwa huru kwa dhamana.

  Iwapo atapatikana na hatia, mbunge huyo anakabiliwa na kifungo cha maisha gerezani.
   

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: