14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 8:34 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  PERES JEPCHIRCHIR,MWANARIADHA WA KENYA AVUNJA REKODI YA DUNIA YA MBIO ZA HALF MARATHON ZA PRAGUE

  Mwanariadha wa Kenya Peres Jepchirchir alivunja rekodi ya dunia ya mbio za half marathon za Prague katika Jamhuri ya Czech kwa upande wa akina dada.

  Mkenya huyo alikimbia umbali huo wa kilomita ishirini na moja nukta moja kutumia saa moja na sekunde tano nukta tatu nne akiivunja rekodi iliyowekwa na mwanariadha wa Ethiopia Netsanet Gudeta mwaka 2018.

  Ndani ya dakika thelathini nukta 32 kwenye mbio hizo, Jepchirchir alikuwa amemaliza kilomita kumi .
  Hii ni mara ya pili kwa Jepchirchir kuweka rekodi duniani ya kukimbia umbali huo. Mwaka 2017, Jepchirchir alikimbia umbali wa kilomita ishirini na moja nukta moja mjini Ras Al Khaimah kwa kutumia saa moja sekunde tano nukta sita, rekodi ambayo hata hivyo ilivunjwa baada ya miezi miwili.

  Wakati uo huo Mkenya Kibiwot Kandie aliyeibuka mshindi wa mbio za Prague Half Marathon kwa upande wa wanaume katika Jamhuri ya Czech.

  Katika mbio hizi, nafasi ya kwanza hadi ya kumi zilitawaliwa na Wakenya ambapo Kandie aliwaongoza.
  Kibiwot alitumia muda wa dakika hamsini na nane nukta saba saba kumaliza mbio hizo za kilomita ishirini na moja, akifuatwa na Mkenya mwingine Philemon Kiplimo Kimaiyo kwa karibu aliyetumia muda wa dakika hamsini na tisa nukta tano sita.
  Benson Kipruto ambaye vilevile ni Mkenya alimaliza katika nafasi ya tatu kwa kutumia saa moja nukta sita kumaliza umbali huo.Wengine ni Amos Kurgat aliyemaliza katika nafasi ya nne, Felix Kipkoech ambaye alimaliza katika nafasi ya tano, Timothy Kibet Kosgei aliyemaliza katika nafasi ya sita vilevile Barnerd Kimeli aliyemaliza katika nafasi ya saba.Na Alfred Chelal alimaliza katika nafasi ya kumi kwa kutumia saa moja, sekunde moja nukta tatu mbili.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: