14.8 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 8:34 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  POLISI WAUANA KISA CHAKULA CHA JIONI

  Maafisa wawili wa polisi katika kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya walifariki dunia saa chache baada ya kupigania msichana waliomtaka wote wawili.Msichana huyo pia ni afisa wa polisi eneo hilo.

  Kulingana na ripoti ya polisi, kisa hicho kilitokea katika nyumba za maafisa wa gereza la Mwea ambapo mmoja wa maafisa hao, Kering Kipkosgei, alikuwa amealikwa nyumbani kwa mwenzao wa kike kwa chakula cha usiku.

  Afisa Bonface Mithamo, ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na afisa huyo wa kike alifika nyumbani kwa msichana huyo na kumpata mwenzake.

  Mithamo alitaka kujua ni kwa nini Kipkosgei alikuwa katika eneo hilo na ndipo vita vikazuka.

  Mithamo alimpa kichapo kikali kabla ya Kering kuamua kutumia silaha yake kujiokoa ambapo alimpiga risasi shingoni.

  Kwa mujibu wa gazeti la Standard la Kenya,liliripoti kwamba baada ya Kering kuona alivyo mjeruhi Mithamo, aligeuza bunduki na kujipiga risasi.

  Wawili hao walifariki walipokuwa wakipelekwa hospitali huku afisa wa kike aliyekuwa akizozaniwa akisema alijaribu awezalo kumaliza vita dhidi yao ila hakufanikiwa.

  Maafisa wa polisi waliofika kwenye nyumba hiyo walipata bastola moja na risasi 11.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: