Radi imewaua watoto wawili wakike wa familia moja na kuwajeruhi baba na mama wakazi wa kijiji cha Shasya nchini Tanzania katika nyumba tatu tofauti.
Hilo tukio limetokea leo majira ya saa saba mchana na kusababisha vifo vya watoto hao waliofahamika kwa majina ya Edina Mgale,mwanafunzi wa darasa la sita na Miznala Mgale mwenye umri wa miaka minne.
“Mimi na mtoto mmoja tulikuwa kwenye nyumba kubwa na marehemu alikuwa kwenye nyumba nyingine.Mama na watoto wengine walikuwa jikoni na baada ya kusikia mlio wa radi ndipo nilianza kuita na kukuta mama amezirai,” amesema Mawazo Mgale ambaye ni baba mzazi wa Marehemu.
Nae diwani wa kata ya Halungu nchini humo Maalifa Mwashitete,amewatoa hofu wananchi kuacha kuhusisha tukio hilo na imani za kishirikina.