Kinara wa chama cha ODM nchini Kenya,Raila Odinga ameonekana kwa mara ya kwanza kabisa tangu asafiri kimya kimya kwenda Dubai alikolazwa huku madai mbalimbali yakienezwa mitandaoni kuhusu hali yake ya afya.Kutokana na video ambayo mwanawe winnie Odinga amemrekodi akiwa amevalia suruali ya buluu na shati ya maanjano. Raila ameonekana wazi na kueleza anavyoendelea vyema baada ya kufanyiwa upasuaji.
Kiongozi huyo ameonekana kuwa mwenye tabasamu huku akinyoosha Mikono kama mtu anayefanya mazoezi.Hii hapa sauti yake na mwanawe Winnie Odinga.
Pia hajasahu kuwashukuru wafuasi wake na wote waliomtakia afueni ya haraka
Raila alikuwa na tatizo la mguu lililomsababishia uchungu sehemu nyingine za mwili na kupelekea kufanyiwa upasuaji na hii iliwekwa wazi na mkewe Bi Ida Odinga wakati akihojiwa kwenye gazeti la standard.