14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 6:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  RAIS KENYATTA: MWENYEKITI MPYA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

  Rais  Uhuru Kenyatta wa Kenya amekabidhiwa uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Februari 27,2021.

  Rais Kenyatta amekabidhiwa uenyeketi huo baada ya mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo kufanyika kwa njia ya mitandao.Amechukua hatamu yake kutoka kwa mwenyekiti anayeondoka,Rais wa Rwanda,Paul Kagame.

  Pia aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la nchi za Afrika Mashariki. Dkt. Peter Mathuki ambaye ni raia wa Kenya aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa jumuiya hiyo akichukua nafasi ya Balozi Liberate Mfumukeko raia wa Burundi ambaye amekamilisha muhula wake.

  Vilevile mmoja wa majaji wapya wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki, Kathurima M’Inoti aliapishwa.

  Kwenye mkutano huo, pia viongozi wa nchi wanachama walisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana na kudumisha amani.

  Hata hivyo,Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inayaleta pamoja mataifa matano ya Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi. Jumuiya hiyo iliasisiwa mwaka 1967, ikavunjika mwaka 1977 na kufufuliwa upya Julai 7, 2000. Hivyo mkutano huo uliofanyika Februari 27,2021 ulikuwa wa 21.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: