Hafla ya kumuapisha Lazarus Chakwera kuwa rais mpya wa Malawi imefanyika katika mji mkuu wa Lilongwe baada ya kiongozi huyo kushinda katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne wiki iliyopita.Hii ni baada ya Mahakama ya Malawi kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka jana kutokana na dosari zilizokumba uchaguzi huo.
Bwana Chakwera alimshinda aliyekuwa rais wa nchi hiyo Peter Mutharika kwa asilimia 58.57 ya kura katika uchaguzi wa Jumanne, tume ya uchaguzi ilitangaza usiku wa Jumamosi.
Japo Malawi ni nchi ya pili barani Afrika baada ya Kenya kurudia uchaguzi wa rais baada ya matokeo ya awali kupingwa mahakamani, imekuwa nchi ya kwanza kwa mgombea wa upinzani kushinda duru ya pili ya uchaguzi.
Ushindi wa Chakwera unaendelea kutoa matumaini mapya kwa uhuru wa mahakama barani Afrika, na umuhimu wa kuwa na tume na mifumo huru ya uchaguzi.
Kama ilivyotokea Malawi nchini Kenya upinzani ulipinga matokeo ya uchaguzi wa urais mwaka 2017 na kushinda mahakamani.
Hata hivyo mgombea wa upinzani Raila Odinga alisusia duru ya pili ya uchaguzi lakini kwa Malawi,Rais mteule Lazarus Chakwera akipiga kura .
Kwa upande wa familia, Chakwera na mkewe Bi Monica Chakwera wana watoto wakubwa wanne pamoja na wajukuu kadhaa.