Rais Uhuru Kenyatta amepokea hati za utambulisho za Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Stephen Simbachawene.
Rais Kenyatta amepokea hati za utambulisho za Balozi huyo wa Tanzania nchini Kenya, Balozi Simbachawene kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Rais jijini Nairobi nchini Kenya.ambapo pamoja na mambo mengine,
Pamoja na mambo mengine,Balozi Simbachawene amemhakikishia Rais Kenyatta kuwa ataendelea kuboresha mahusiano ya nchi hizo mbili za Tanzania na Kenya, kukuza biashara baina ya nchi hizo kwa kuboresha diplomasia ya uchumi kwa ujumla wake.