Rais Uhuru Kenyatta amewataka mawaziri wote pamoja na makatibu katika wizara kuchukua likizo ya mapumziko ya lazima huku kukiwa na taarifa za mabadiliko kwenye baraza la mawaziri.
Rais Kenyatta amesema kuwa mawaziri na makatibu watalazimika kushughulikia majukumu ya dharura.
Kwa mujibu wa barua iliyotumwa na mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kinyua likizo hiyo ya siku 14 ambayo imeanza leo Agosti 17, ambapo mawaziri hawatafanya ziara za kukagua miradi na mipango ya serikali.
Likizo hiyo ya mawaziri na makatibu inakuja huku kukiwa na taarifa kuhusu Rais Kenyatta kuifanyia mabadiliko baraza la mawaziri.