14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 6:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  RAIS WA KENYA,UHURU KENYATTA AITISHA MKUTANO WA MASENETA KWA MARA YA KWANZA


  Raisi uhuru Kenyatta anatarajiwa kuandaa mkutano na maseneta wa chama cha jubilee,huku wengi wa wachanganuzi wa kisiasa wakisema utakuwa ni wa kulenga Kipchumba murkomen kama kiongozi wa wengi na susan kehika kama kiranja wa wengi,kwani wawili hao wamekuwa wakionekana kama waasi na wamekuwa wakikashfikiwa pakubwa kwa kumrushia cheche za maneno rais Uhuru Kenyatta licha ya kuwa wanahudumu katika nafasi hizo.
  Huu utakuwa ni mkutano wa kwanza wa maseneta tangu chama cha jubilee kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 huku naibu kiranja Irungu Kang’ata akitumiwa kupitisha ujumbe huo wa mkutano kwa maseneta kinyume na ilivyo kawaida kuwa kiranja Susan Kehika ndio anafaa kufanya hivyo.
  Japo ujumbe waliotumiwa maseneta wa Jubilee na wale wa KANU ambao wako kwa muungano mmoja hawajasema ajenda kamili ya mkutano huo.Aidha Chama cha Jubilee kimekuwa kikipitia mawimbi makali ya kisiasa huku tofauti kati ya Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto zikileta joto katika chama hicho.kwa hivyo wengi wanahisi huo ni mkutano wa kutimua viongozi wa senate ambao wamekuwa wakosoaji wakuu wa rais.Murkomen na kehika wakiangaziwa kuwa wamekuwa wakionekana kama waasi kwenye chama hicho.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: