18.4 C
Nairobi
Saturday, May 8, 2021
Kenya
162,666
Total confirmed cases
Updated on May 8, 2021 10:17 am

GAVANA WA ZAMANI WA NAIROBI MIKE SONKO AACHILIWA KWA DHAMANA

Hatimaye aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ameachiliwa kwa dhamana baada ya kuzuiliwa rumande kwa muda wa takribani mwezi mmoja. Kwa mujibu wa TUKONEWS, Sonko...
More

  Latest Posts

  RAIS WA TANZANIA, MH.JOHN POMBE MAGUFULI AFARIKI DUNIA

  Rais wa Tanzania Mh John Pombe Joseph Magufuli amefariki dunia Machi 17,2021 majira ya saa kumi na mbili jioni.Habari za kifo chake kimetangazwa na Makamu wa Rais wa Tanzania,Mama Samia Suluhu.

  Kifo chake kimetokana na maradhi ya moyo.Amefariki akipokea matibabu katika hospitali ya Mzena jijini Dar es salam nchini Tanzania.

  Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania, hakuonekana mbele ya umma kutoka Februari 27,2021 licha ya uvumi ulioenea kwamba anaumwa, serikali ya Tanzania haikuweka wazi aliko Rais huyo mpaka wakati Makamu wake ametangaza kuhusu kifo chake kupitia kwa Runinga ya Taifa hilo ya TBC.

  Yuko wapi Rais Magufuli? swali la YUKO WAPI RAIS MAGUFULI ndilo lililoulizwa sana na wengi ambapo liliishia kwa watu kukamatwa.

  Kifo cha Rais Magufuli kinakuja wakati ambapo Tanzania imeshuhudia vifo na kile kinachoitwa “magonjwa ya kupumua” kuyakumba majina makubwa ya kisiasa nchini humo. Ila wiki moja kabla kuonekana kwake, Magufuli alikiri kwamba virusi vya corona, vinasambaa nchini mwake hasa baada ya kifo cha makamu wa rais wa Zanzibar, Maalim Seif ambaye baadae iliripotiwa kwamba alifariki kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: