22.8 C
Nairobi
Friday, October 15, 2021
Kenya
251,669
Total confirmed cases
Updated on October 14, 2021 9:34 pm

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  RAIS WA ZAMANI WA UFARANSA NICOLUS SARKOZY AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 3

  Aliyekuwa Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu baada ya kukutwa na hatia ya ufisadi na kueneza ushawishi.

  Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama mjini Paris leo Machi 1,2021,  inajumuisha mwaka mmoja gerezani na miaka miwili ya kifungo cha nje.

  Aliyekuwa Rais wa Ufaransa akiingia mahakamani kuskiliza hukumu yake.

  Sakorzy mwenye umri wa miaka 66, alihudumu kwa muhula mmoja tu kati ya mwaka 2007 na 2012,  alikuwa anashtakiwa kwa kujaribu kupata taarifa za ndani kinyume cha sheria kuhusu uchunguzi juu ya ufadhili wa kampeni zake kutoka kwa jaji Gilbert Azibert mwaka 2014.

  Uchunguzi wa mahakama pia ulionyesha kwamba Sarkozy alikuwa anatumia nambari ya simu isiyo rasmi kuwasiliana na Jaji huyo kwa ajili ya kupata habari ya ndani juu ya uchunguzi juu ya fedha zake za kampeni na alimuahidi kumtafutia kazi nzuri zaidi nchini Monako. Jambo ambalo hakutimiza.

  Mahakama hiyo imesema Sarkozy atakuwa na haki ya kuomba kuzuiliwa nyumbani na hivyo atafungwa bangili ya umeme mguuni kumzuia asitoke nyumbani.

  Pia, wakili Thiery Herzog na jaji Gilbert Azibert ambao ni washtakiwa wenzake  wamekutwa na hatia na wamehukumiwa kifungo sawa na chake.

  Sarkozy atakabiliwa na kesi nyingine baadae mwezi huu, pamoja na watu wengine 13 kwa mashtaka ya kufadhili kinyume cha sheria kampeni yake ya urais mwaka 2012.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: