Rapper wa Marekani Lil Uzi Vert (26) ametangaza kutumia USD 24.M kununua almasi na kuibandikiza kwenye paji la uso.
Baada ya kuwekwa almasi hiyo kwenye paji la uso wake ilimfanya avuje damu mwanzoni na akaipost hiyo picha lakini baadae aliifuta na kisha kupost video akiwa anacheza huku akiwatoa hofu mashabiki wake kwamba yuko sawa.
Lil Uzi amekiri kwamba USD Milioni 24 hizo sio pesa alizitoa kwa siku moja bali alianza kulipia kidogokidogo toka mwaka 2017.