16.1 C
Nairobi
Sunday, September 26, 2021
Kenya
248,392
Total confirmed cases
Updated on September 26, 2021 8:39 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  RUSSIA YATANGAZA CHANJO YA KWANZA YA CORONA DUNIANI

  Rais Vladmir Putin wa Russia ametangaza kusajiliwa kwa chanjo ya kwanza ya Virusi vya Corona duniani.Putin amesema kwamba baada ya majaribio kadhaa inaonyesha kwamba chanjo hiyo inaongeza kinga mwilini ili kukabili makali ya virusi hivyo.
  Putin amechukua hatua hiyo baada ya wizara ya afya kuidhinisha chanjo hiyo iliyofanyiwa utafiti kwa miezi miwili katika maabara mjini Moscow.

  Rais Vladimir Putin amesema kuwa tayari binti yake mmoja amepewa chanjo hiyo inayozuia kuambukizwa virusi vya corona na maradhi ya COVID-19.

  Rais wa Russia amesema kuwa chanjo hiyo imevuka awamu zote za majaribio.

  Wiki kadhaa zilizopita Naibu Waziri wa Afya wa Russia, Olek Grenev alikuwa ametangaza kuwa, chanjo hiyo imeingia katika majaribio ya mwisho.

  Vilevile mwezi uliopita afisa mmoja wa ngazi za juu wa Wizara ya Afya ya Russia alitangaza kuwa inatarajiwa kwamba chanjo ya virusi vya corona itaanza kuzalishwa kwa wingi nchini humo mwezi Septemba mwaka huu.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: