19.4 C
Nairobi
Saturday, October 16, 2021
Kenya
251,669
Total confirmed cases
Updated on October 14, 2021 9:34 pm

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

  Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka 99 baada ya kuugua kwa muda.

  Kifo cha Sarah kimethibitishwa na binti yake Marsat siku ya leo Jumatatu, Machi 29,2021.

  Marehemu alikuwa mke wa tatu wa Hussein Onyango Obama, ambaye ni babu yake Barack Obama kwa upande wa mzazi wa kiume wa raisi huyo wa zamani wa Marekani.

  Rais huyo wa 44 wa taifa hilo lenye ushawishi mkubwa duniani, alimtembelea bibi yake mara ya mwisho mnamo Julai 2018 wakati wa ziara yake nchini Kenya.

  Picha ya Barack Obama na bibi yake,Sarah Obama. Obama alipomtembelea bibi yake nchini Kenya mwaka 2018

  Sarah Obama alikuwa anaishi katika kijiji cha Nyang’oma Kogelo,maili 30 kutoka mjini Kisumu karibu na Ziwa Victoria.

  Kwa mujibu wa Sheikh Musa Ismail ambaye pia ni msemaji wa familia ya Mama Sarah Obama ni kwambamarehemu Sarah Obama atazikwa kesho Machi 30,2021.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: