Seneta wa Nairobi nchini Kenya,Johnson Sakaja amekesha kwenye korokoro ya polisi baada ya kukamatwa usiku wa kuamkia leo kwenye club ya burudani jijini Nairobi.
Polisi wamesema walimkamata Seneta sakaja akiwa kwenye club ya burudani kwa jina lady’s Lounge wakati wa curfew katika barabara ya Dennis Pritt. Polisi wamesema walimkuta saa nane usiku akilewa akiwa ndani ya kundi la watu wengine kumi ndani ya club hiyo..Na sakaja akajaribu kuwazuia kumkamata Pamoja na wenzake hao huku akiwatisha polisi lakini walichukuliwa wote kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kilimani kilichopo Nairobi ambako wamekesha korokoroni .
Katika video ambayo tumeipata kwenye mitandao ya kijamii ,Sakaja anajaribu kuzungumza na maafisa wa polisi ambao wamempa kisogo huku akiwauliza wampe simu yake huku akiwa ameshikilia chuma yaani ‘behind the bars.’
Hadi wakati tukipost hii habari Seneta Sakaja alikuwa ameachiliwa huru huku akijitokeza na kukana madai kwamba alikamatwa na kukesha kwenye korokoro ya polisi usiku wa leo.Kupitia kwa mtandao wake wa Twitter amesema habari hizo kuwa ni za uongo.Akiwauliza waliotoa habari hiyo watoe nambari ya polisi ya OB inayothibitisha kuwa alikamatwa na kutiwa ndani kwenye kituo cha Kilimani.
Ujumbe huo wa twitter wa Seneta Sakaja umezua mjadala mkali kwenye mtandao ikizingatiwa ni yeye ndiye mwenyekiti wa kamati ya Senate iliyopewa jukumu la kutoa muongozo kwa serekali kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Msikilize Seneta Sakaja akifoka apewe simu yake akiwa korokoroni