16.1 C
Nairobi
Sunday, September 26, 2021
Kenya
248,392
Total confirmed cases
Updated on September 26, 2021 9:40 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  TANZANIA YAONDOA MARUFUKU YA SAFARI ZA NDEGE ZA KENYA AIRWAYS KUTUA NCHINI HUMO

  Tanzania imeondoa marufuku ya safari za ndege za Shirika la Kenya Airways kuingia kwenye anga yake iliyokuwa imewekwa.

  Marufuku hayo yameondolewa siku moja tu baada ya serikali ya Kenya kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, KCAA, kutoa orodha ya nchi 147 ikiwemo Tanzania na kutangaza kwamba raia wa nchi hizo hawatashurutishwa kuwekwa karantini ya siku 14 baada ya kuwasili nchini Kenya kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya korona.

  Hii ni awamu ya tatu ambapo Kenya imefungua anga zake kwa safari za ndege za kamataifa baada ya kufungwa kufuatia janga la korona mapema mwezi Machi mwaka huu.Ikumbukwe kuwa Kenya ilirejelea safari zake za ndege za kimataifa Agosti tarehe mosi kwa mataifa kumi na moja pekee ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya korona.

  Agosti 19, orodha ya mataifa yaliongezwa na kufikia 130 japo Tanzania ikafungiwa nje tena huku serikali ikisema kwamba itaendelea kuongeza idadi ya mataifa kutokana na hali ya maambukizi.

  Hatua ya Kenya kutoijumulisha Tanzania kwenye Orodha hiyo ilizidisha uhasama ambao umekuwepo kwa muda huku madereva wa matrela wa Kenya wakilazimika kupimwa mara mbili kabla ya kuingia Tanzania na hata wengine kuzuiwa kuingia nchini humo.

  Taarifa hiyo ya Tanzania kuruhusu ndege za Kenya Airways imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: