Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba China inampango wa
kutumia kila njia ili kumfanya asichaguliwe tena kwenye uchaguzi mkuu
wa Urais unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Katika mahojiano yaliofanyika katika Ikulu ya Whitehouse na chombo cha
habari cha Reuters, amesema kwamba China inakabiliwa na athari chungu
nzima kutoka kwa Marekani kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
Anasema China ilificha kuhusu ugonjwa wa Corona na hivyo kuufanya
usambae dunia nzima na kuleta madhara makubwa.
Hata hivyo, Trump amekuwa akikosolewa vikali kwa Jinsi anavyokabiliana
na tatizo hilo.
Mlipuko wa virusi vya corona umeharibu uchumi wa Marekani ambao
Trump alikuwa akiutumia kama kinga kujipigia debe ili kuchaguliwa tena
katika uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka huu.
Ambapo alisikika akisema kuwa China inafanya kila mbinu za kutaka
ashindwe katika uchaguzi ujao. Wanataka mpinzani wake mkuu kutoka
chama cha Democrat Joe Biden ndo ashinde uchaguzi wa mwezi Novemba.
Aidha, Trump amepinga vikali utafiti uliofanyika nchini humo na kutoa
maoni kwamba mpinzani wake Biden ana asilimia kubwa za kuibuka
shindi.
Photo courtesy of motherjones.com