14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 7:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  TUME YA UCHAGUZI NCHINI KENYA {IEBC} YATANGAZA TAREHE RASMI YA CHAGUZI NDOGO KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI

  Vyama vya kisiasa vimeanza kujitayarisha tena kwa chaguzi ndogo zitakazofanyika kwenye maeneo mbalimbali nchini mwezi Mei 2021.

  Tayari Tume ya Uchaguzi IEBC imesema kwamba uchaguzi mdogo wa Useneta kwenye Kaunti ya Garissa, eneo Bunge la Bonchari ,eneo bunge la Juja na wadi ya Ruuri kwenye Kaunti ya Nyandarua utafanyijka Mei 18,2021.

  Vyama vya kisiasa vina hadi tarehe 22 mwezi huu kuwasilisha katika IEBC majina ya wagombea wake. Aidha kampeni za chaguzi hizo ndogo zitaanza Machi tarehe 29 hadi Mei tarehe 15 2021.

  Kufuatia hayo, Bodi ya Uchaguzi ya Chama cha ODM imewataka walio na nia ya kuwania nyadhifa hizo kupitia chama hicho kutuma maombi yao kabla ya tarehe 11 mwezi huu yaani siku ya Alhamisi. Wameshauriwa kuzipata fomu za kutuma maombi hayo kwenye ofisi za makao makuu ya ODM jijini Nairobi au kupitia mtandao rasmi wa ODM.

  Huku watakaotaka kupeperusha bendera ya UDA katika chaguzi hizo ndogo wana hadi kesho saa sita mchana kutuma maombi.

  Uchaguzi mdogo wa Garissa  unafuatia kifo cha Seneta Yusuf Haji tarehe 15 Februari. Aliaga dunia akiwa na miaka 80 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

  Kiti cha Bonchari kiliachwa wazi kufuatia kifo cha John Oroo Oyioka baada ya kuugua kwa muda mrefu.

  Ni mwezi jana pia ambapo aliyekuwa Mbunge wa Juja Francis Munyua Waititu, maarufu Wakapee alifariki dunia,hivyo eneo hilo la bunge halina mbunge anayewawakilisha kwa sasa.

  Wakapee aliaga dunia baada ya kuugua saratani ya ubongo kwa muda mrefu.

  Alhamisi iliyopita IEBC ilifanya chaguzi ndogo saba kwenye maeneo mbalimbali nchini huku baadhi zikikumbwa na ghasia jambo linalotia wasiwasi wakati huu taifa linapojiandaa kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: