Uingereza ni kati ya mataifa yanayochunguza chimbuko la corona yaani covid 19 ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kwamba inahusishwa na maabara moja ya Uchina iliyokuwa ikiendeleza utafuiti wa magonjwa ndani ya wanyama na inakisiwa kwamba virusi vya corona vilichipuka vyenyewe tu na wala sio kutoka kwenye maabara baada ya kutengenezwa na binadamu .lakini hiyo haimaaanishi kwamba ugonjwa huo haukutokea kimakosa kwenye maabara katika mji wa Wuhan katika jimbo la Hubei nchini Uchina,Sehemu ambayo kisa cha kwanza kiliripotiwa.Idara ya ujasusi ya marekani inachunguza uwezekano wa virusi hivyo kuchipuka kimakosa kutoka maabara iliyokuwa ikichunguza magonjwa ya wanyama.