Je,unajua kwamba nchi ya Ethiopia ndio imeingia mwaka wa 2013 wakati nchi zingine zimefika mwaka 2020?
Ndio ,Ethiopia sasa hivi bado inasherehekea mwaka mpya kwani imeingia mwaka mpya siku 6 zilizopita.Yaani Mwaka wa 2013.Mwaka mpya kwao wanauita Enkutatash. Kulingana na kalenda ya Ethiopia,mwaka wao una miezi kumi na mitatu na kila mwezi una siku 12 isipokuwa mwezi wa 13 ambao una siku 5 na unaitwa Pagumen.
Nchi ya Ethiopia inatumia Kalenda ya kanisa la Roman iliyorekebishwa mnamo miaka ya 525 AD.Hivyo wananchi wa Ethiopia walisherehekea millennia mpya tarehe 11 Mwezi wa tisa,mwaka 2007.
Nchi hiyo iko nyuma ya Kenya na nchi nyingi kwa miaka 71/2.