22.8 C
Nairobi
Friday, October 15, 2021
Kenya
251,669
Total confirmed cases
Updated on October 14, 2021 9:34 pm

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  VIFO VYA CORONA MAREKANI VYAFIKA 85,197

  Vituo vya kuzuia na kudhibiti magonjwa nchini Marekani (CDC) vimetangaza vifo vipya 1,426 vinavyohusiana na ugonjwa wa Covid 19 , na kufikisha jumla ya watu 85,197 waliofariki dunia tangu kuzuka kwa janga hilo.

  Vituo vya CDC pia vimeripoti visa vipya 21,647 vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19, na kufikisha jumla ya idadi ya visa 1,430,348 vya maambukizi nchini humo.

  Hayo yanajiri wakati Ulaya imeanza kuchukua hatua za awali kuelekea kufungua mipaka yake ya ndani,baada ya miezi miwili ya vizuizi vya kukabiliana na janga la covid-19.

  Aidha,Shirika la Afya Duniani WHO limesema kwamba huenda ikawa vigumu kuukabili ugonjwa wa Covid-19 ambao sasa umewaathiri zaidi ya watu milioni nne kote duniani.Katika mkutano na  waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka Geneva,Mkurugenzi wa dharura  wa WHO Mike Ryan,  amesema mataifa mbalimbali yanastahili kuweka mikakati kuhusu jinsi ya kukabili maambukizi zaidi jinsi ambavyo virusi vya HIV vimeendelea kukabiliwa na kuonya dhidi ya kujaribu kubashiri ni lini virusi vya corona vitatoweka.

  Kufikia sasa kuna zaidi ya chanjo mia moja zinaendelea kushughulikiwa na wanasayansi kwenye mataifa mbalimbali kuangamiza ugonjwa wa Covid 19.

  Ryan amesema kuna magonjwa mengi yaliyo na chanjo ila hayajaangamizwa,kama vile ukambi,akisema huenda ikachukua muda kwa suluhi ya kudumu kupatikana kwa hivyo mataifa yachukue tahadhari ya hali ya juu.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: